Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 November 2014
Sunday, November 02, 2014

Real Madrid haikamatiki kwa sasa.


Na Oscar Oscar Jr

Real Madrid wameendeleza wimbi la ushindi baada ya hapo jana kuiadhibu, Granada kwa mabao 4-0. Christiano Ronaldo aliendeleza ubora wake katika kuzifumania nyavu ambapo jana aliweza kufunga katika dakika za awali kabisa na kufikisha bao lake la 17 msimu huu.

Real Madrid ambao walianza ligi kwa kusua sua kufuatia kuwakosa Angel Di Maria aliyejiunga na klabu ya Manchester United na kiungo Xaib Alonso aliyetimkia Bayern Munich, sasa wanaonekana kutulia. 

Taratibu wachezaji wapya, James Rodriguez, Toon Kroos wameingia kwenye mfumo wa kocha Carlo Anchelotti na matunda yameanza kuonekana.

Baada ya kuwafunga Barcelona wiki iliyopita kwa magoli 3-1, Real Madrid baada ya ushindi wa jana wamefikisha pointi 24 na kukaa kileleni mwa msimamo wa La Liga baada ya wapinzani wao timu ya Barcelona kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Celta Vigo.

Karim Benzema, Christiano Ronaldo walifunga bao moja kila mmoja huku, mfungaji bora wa kombe la Dunia, James Rodriguez akifunga mabao mawili na kukamilisha ushindi huo kwa vijana wa Carlo Anchelotti.

Granada ambao wamefunga magoli sita pekee kwenye msimu huu huku wakiruhusu kufungwa mabao 17 mpaka sasa, walijikuta kwenye wakati mgumu kuipenya safu ya ulinzi ya Real Madrid iliyoongozwa na beki Sergio Ramos. 

Kipa na Nahodha Iker Casillas muda mrefu alijikuta amekaa tu kwa sababu hakukuwa na mashambulizi yoyote ya hatari langoni mwake.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!