Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 November 2014
Sunday, November 02, 2014

Bayern Munich 2-1 Borussia Dortimund


Na Oscar Oscar Jr

Bado mambo yameendelea kuwa magumu kwa Borussia Dortimund baaada ya hapo jana kujikuta wakikubali kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa wapinzani wao, Bayern Munich kwenye dimba la Allianz Arena. 

Bayern ambao wanaongoza ligi ya Bendesliga kwa pointi 24, walipata magoli yao kupitia Robert Lewandowski na Arjen Roben aliyefunga kwa mkwaju wa Penalty.

Dortimund ambao wameshinda michezo miwili tu na kutoka sare moja msimu huu, walikuwa na wakati mzuri sana kipindi cha kwanza huku beki wa kati na nahodha wao, Mats Hummels akionekana kumnyima nafasi Lewandowski ya kuwaadhibu. 

Marco Reus kama kaida yake, ndiye aliyekuwa mfungaji wa bao la Dortimund ingawa unga ulizidi maji kipindi cha pili. Hummels alipata maumivu kwenye mchezo huo na kushindwa kurudi kwenye kipindi cha pili huku Neven Sabotic akichukuwa nafasi yake. 

Kocha wa Bayern Munich, Pep Gaudiola alifanya mabadiliko ya kumtoa Mario Gotze na kumuingiza Frank Ribery na hapo ndipo Dortimund waliposhindwa kwenda sambamba na kasi ya winga huyo wakifaransa.

Sabotic alijikuta akiruhusu bao la kwanza baada ya kushinda kuondoa mpira vizuri eneo lao na kusababisha mpira huo kunaswa na Lewandowski ambaye alipiga moja kwa moja na kupata bao la kusawazisha. 

Sabotic pia alijikuta kwenye hali ngumu baada ya kuzidiwa kasi na Frank Ribery ambaye alikuwa anamtafuta kipa kwenye box na kujikuta akimwangusha. Mwamuzi aliamuru ipigwe penalty ambapo, Arjen Roben alifunga kwa ustadi mkubwa.

Bayern Munich sasa wanajichimbia kileleni mwa Bundesliga wakiwa na pointi 24 baada ya kushuka dimbani mara 10 huku Borrusia Dortimund wakiendelea kubaki na alama saba na kuwa kwenye mstari wakushuka daraja. 

Pamoja na kucheza vizuri hasa eneo la kati, bado Dortimund wanategemea ubora wa kiungo wa Marco Reus hasa kwenye mechi kubwa kuweza kubadili matokeo tofauti na Bayern ambayo imesheheni watu wa kubadili mchezo muda wowote.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!