Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 November 2014
Monday, November 03, 2014

Nahodha wa Yanga kuukosa mchezo dhidi ya Azam


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya timu ya Yanga kuhitimisha ziara yao ya michezo ya ligi kanda ya ziwa, wamefanikiwa kupata pointi tatu kwenye michezo miwili huku wakishinda bao 3-0 dhidi ya Stand United ya Mkoani Shinyanga na kisha, kuchapwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar ya mkoa wa Kagera.

Katika mchezo huo, Yanga walipata mapigo mawili. Kwanza ni kupoteza mchezo huo, hayakuwa matokeo mazuri kwao na pili, ni kumpoteza moja ya wachezaji bora kwa sasa kwenye kikosi chao, Nahodha Nadir Haroub baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.

Ukitazama ratiba, unagundua kuwa Cannavaro ataukosa mchezo wao dhidi ya Mgambo JKT na mchezo dhidi ya Azam mechi hizo zote zikipigwa kwenye dimba la Taifa, Dar es Salaam. Cannavaro ni moja ya wachezaji tegemeo kwa sasa wa Yanga na kukosa michezo hiyo ni pigo.

Yanga kwa sasa wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 10 nyuma ya Azam nao wakiwa na alama 10 huku, Coastal Union wakisalia kwenye nafasi ya pili wakiwa na alama 11 na Mtibwa Sugar, wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 14 kwenye michezo sita iliyochezwa mpaka sasa.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!