Searching...
Image and video hosting by TinyPic
3 November 2014
Monday, November 03, 2014

Simba kusaka mshambuliaji dirisha dogo.



Na Oscar Oscar Jr

Baada ya timu ya Simba kucheza michezo sita na kufunga magoli sita, Uongozi wa Simba unataka kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kwa kufanya usajili wa mshambuliaji mwingine kutoka nje ya nchi. 

Gazeti la Champion la leo, limeeleza kuwa Simba wameanza mazungumzo ya kuwapata wachezaji watatu huku mmoja akiwa ni mshambuliaji.

Ukiachana na Paulo Kiongera, mshambuliaji wa Simba kutoka nchini Kenya, timu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam ina Elius Maguli, Emmanuel Okwi na Amis Tambwe ambaye pamoja na kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu msimu uliopita akifunga magoli 19, chini ya kocha mpya Patrick Phiri Star huyo wa Burundi amepoteza namba.

Moja kati ya washambuliaji wanaotajwa kusajiliwa Simba ni  mshambuliaji wa klabu ya TP Mazembe, Jerome Ramathakwane amabaye ni raia wa Botswana.

Mchezaji huyo alikuja kufanya majaribio kabla ya msimu huu kuanza kwenye klabu ya Simba na baadaye, uongozi ukavutiwa zaidi ya Kiongera.

Simba inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu huku ikiwa haijashinda hata mchezo wake mmoja. Siku ya Jumamosi ijayo timu hiyo itakuwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kucheza na Ruvu Shooting huku ikiwa na mzigo mkubwa wa kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kupata ushindi wao wa kwanza msimu huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!