Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 February 2015
Friday, February 06, 2015

Ronaldo kurejea leo katika" Madrid derby"




Na Florence George


Mabingwa watetezi, klabu ya soka ya Athletico Madrid itashuka dimbani leo hii kumenyana dhidi ya mahasimu wao wa karibu klabu ya Real Madrid katika mechi ya ligi kuu nchini Hispania,mchezo huo maarufu kama "Madrid derby" utapigwa katika dimba la Vicente Calderon.

Real Madrid haijaifunga Athletico tangu msimu uliopita  katika fainali ya ligi ya mabingwa ulaya,amabapo msimu huu timu hizo zimeshakutana mara tano huku Athletico ikishinda michezo mitatu na kutoa sare mbili. 


Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anatarajiwa kurejea dimbani katika mchezo baada ya kufungiwa kucheza michezo miwili lakini timu hiyo itakuwa bila ya beki wao wa kati Pepe na Sergio Ramos ambao wote ni majeruhi.

Ronaldo ambaye hadi sasa ameshafunga magoli 28 katika ligi kuu alikosekana uwanjani baada ya kumpiga kofi mchezaji wa Real Sociedad, Jose Angel Crespo pindi timu hizo zilipokutana mwaka huu na kutolewa nje kwa kadi nyekundu na kukumbana na adhabu hiyo.

Pia Real itawakosa wachezaji wake Luka Modric na James Rodriguez ambaye aliumia mguu katika mchezo uliopita dhidi ya Sevilla ambapo anatarajiwa kufanyiwa oparasheni mapema mwezi huu.


Rea Madrid iliyo nafasi ya kwanza itashuka dimbani huku ikiwa inawazidi Athletico iliyo nafasi ya tatu pointi saba na itakuwa inahitaji ushindi iliiweze kuendelea kuwa juu ya Fc Barcelona iliyo nafasi ya pili.





0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!