Na Chikoti Cico
Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas ana hatihati ya kukosekana kwenye michezo miwili inayokuja ya klabu hiyo ndani ya ligi kuu nchini Uingereza baada ya kuumia ukano wa mvungu wa goti (hamstring) kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Capital one dhidi ya Liverpool wiki iliyopita.
Kiungo huyo ambaye mpaka sasa anaongoza kwa kupiga pasi za magoli (assists) kwenye ligi kuu nchini Uingereza alikosekana kwenye mchezo wa Chelsea dhidi ya Manchester City Jumamosi iliyopita.
Na inawezekana akakosekana kwenye mchezo wa wikendi hii dhidi ya Aston Villa huku pia kukiwa na wasiwasi kama ataweza kuwa fiti kwenye mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Everton utakaopigwa Jumatano ya wiki ijayo kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Kukosekana kwa Fabregas huku pia kukiwa na taarifa za kuumia kwa John Obi Mikel kunaweza kutoa nafasi kwa winga aliyesajiliwa mapema wiki hii kutoka Fiorentina Juan Coudrado kwa ada ya pauni milioni 27 kupata nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza akiwa na jezi za klabu ya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment