Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 January 2015
Monday, January 05, 2015

Wavuta Fegi waongezeka kwenye kikosi cha Arsenal.


Na Chikoti Cico

Kipa wa timu ya Arsenal, Wojciech Szczesny akutwa akivuta sigara kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo dhidi ya Southampton ambapo timu ya Arsenal ilifungwa kwa magoli 2-0 huku kipa huyo akifanya makosa ya kizembe yaliyoipa Southampton ushindi huo, uliochezwa tarehe 1 Januari kwenye uwanja wa St Mary’s.

Szczesny ambaye pia aliwahi kupigwa picha akivuta sigara mara mbili kwenye kipindi cha majira ya joto ya mwaka 2013 amepigwa faini ya kiasi cha pauni 20,000 kwa kosa hilo na kutakiwa kuomba msamaha kwa kosa hilo ambalo lilimkasirisha sana kocha wa Arsenal Arsene Wenger.

Na kwenye wa kombe la FA uliochezwa siku ya Jumapili kati ya Arsenal dhidi ya Hull City, Szczsny hakuwepo hata benchi huku kipa namba mbili wa Arsenal David Ospina akicheza mchezo huo ulioisha kwa Arsenal kushinda kwa magoli 2-0.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!