Na Oscar Oscar Jr
Timu ya Stand United ambayo ilicheza mchezo wake wa mzunguko wa tisa mkoani Morogoro dhidi ya Polis Moro, wanatarajia kuingia ndani ya Jiji la Dar es Salaam hapo kesho baada ya kuweka kambi ya muda mfupi maeneo ya Mlandizi mkoani Pwani.
Akizungumza na mtandao huu, msemaji wa timu hiyo, Bilal amesema kuwa, "Tunatarajia kuingia Dar siku ya Jumatano ikiwa ni kuanza kuzoea mazingira ya jiji hilo kabla ya mchezo watu wa ligi kuu mzunguko wa 10 dhidi ya JKT Ruvu"
Ruvu wanaokamata nafasi ya sita wakiwa na alama 13 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, watajirusha kwenye uwanja wa Awanja wa Azam Complex mahali ambapo mchezo wao wa mwisho kwenye dimba hilo walilala bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.
Stand United ambao hawajapoteza mchezo wowote Ugenini huku wakiwa tayari wamekutana na timu kama Simba, Kagera Sugar na Vinara wa ligi hiyo timu ya Mtibwa Sugar, watashuka dimbani bila ya mchezaji wao tegemeo kwa sasa, Harouna Chanongo ambaye alipata kadi nyekundi kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Polis Morogoro.
0 comments:
Post a Comment