Gerrard aibeba Liverpool kombe la FA.
Na Oscar Oscar Jr
Mabao mawili kutoka kwa Nahodha Steven Gerrard yalitosha kuwapatia ushindi Liverpool wa mabao 2-1 dhidi ya AFC Wimbledon ambao wanashiriki ligi daraja la pili kwenye mchezo wa mzunguko wa tatu wa kombe la FA.
Hii ni mechi ya kwanza tangu Gerrard alipotangaza kuiacha klabu ya Liverpool mwishoni mwa msimu huu na kutimkia kwenye ligi kuu ya nchini Marekani.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amekaririwa kabla ya mchezo huu akisema kuwa, kama Liverpool watafanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe hili la FA, basi ubingwa huo watautoa kama heshima ya kumuaga Steven Gerrard ambaye maisha yake ya soka ameyatumia kwenye klabu hiyo yenye historia Uingereza na Ulaya kwa ujumla.
Katika mchezo huo ambao Liverpool waliutawala kwa asilimia 70 huku wakipiga mashuti 22, ulishuhudia vuta nikuvute baada ya mshambuliaji wa Wimbledon, Adebayo Akinfenwa kusawazisha bao la kwanza.
Liverpool bado walionekana bora kwenye mchezo huo ambapo Rodgers aliweka kikosi chake bora kabisa kilichosheheni nyota wa kikosi ambacho siku zote anawatumia kwenye mechi za ligi kuu.
0 comments:
Post a Comment