Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 January 2015
Wednesday, January 07, 2015

Uchambuzi: Yanga vs JKU robo fainali Mapinduzi Cup.


Na Samuel Samuel
 0652464525

Ukitazama mechi zote ambazo Yanga ilishinda magoli manne , Hans aliruhusu timu nzima ifikirie kushambulia na hiyo ilitokana na uwezo mdogo wa timu hizo hasa nafasi ya kiungo na udhaifu wa mabeki wake wa pembeni. 

Taifa Jang'ombe waliiacha Yanga wafanye watakavyo alikadharika Polisi nayo ilionesha udhaifu mkubwa upande wa kushoto na eneo la kiungo. 

JKU si wakubeza hata kidogo kama kweli Hans anahitaji kutinga nusu fainali kwa ushindi mzuri. Ni timu yenye ulinzi mzuri sana kuliko Jang'ombe na Polisi. 

Simba ilitoa somo kubwa sana kwa Hans Jana. Yanga iliwafumua 4-0 wazanzibari hao na Simba kufanya hivyo hivyo Jana. Hiyo ina maanisha ni timu dhaifu hivyo mdachi huyo ni lazima aje kwa taswira tofauti juu ya JKU. 

Simba SC ilipata shida sana na JKU kwenye makundi kabla ya kupata ushindi dakika za mwishoni kupitia kwa Ndemla. 

 JKU katika mechi zake zote inatumia viungo wakabaji wengi tena wenye uwezo mzuri wa kukaba , kupandisha timu na kumiliki mpira vizuri. Hans asirogwe kabisa kumuanzisha Saidi Juma " makapu" kama alivyofanya kwenye mechi dhidi ya Shaba FC. 

Kiungo huyo alionesha udhaifu mkubwa wa kumiliki kiungo. Salumu Telela akisaidiana na Haruna Niyonzima wanatosha kabisa kupambana na wazanzibari hao. 

 Ili kuuvunja mfumo wa 4-5-1 wa JKU ni lazima Yanga isimame na fomesheni itakayoruhusu viungo watano wa JKU kutawanyika ili kubomoa ngome yao. 

Ni lazima Hans awalazimishe JKU wajilinde kwa man to man ili kuua muunganiko wa timu hasa nafasi ya viungo na mabeki wa kati. Itakuwa mechi nzuri ikionesha vita ya viungo .

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!