Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 December 2014
Monday, December 08, 2014

Falcao kuanzia benchi dhidi ya Southampton




Na Floremce George

Huku kukisubiriwa kwa hamu kubwa mchezo kati ya Southampton dhidi ya Manchester United ,kocha wa Manchester United Mholanzi Louis Van Gaal amesema kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao bado hajawa fiti sawasawa kuanza katika mechi hiyo.

Falcao ambaye yupo kwa mkopo katika klabu hiyo wa mwaka mmoja akitokea katika timu ya Monaco ya nchini Ufaransa amekuwa akisumbuliwa na bega tangu mwezi October hali iliyompelekea kuwa nje takribani mwezi mmoja.

Tangu arudi akitokea kwenye majeraha hayo Falcao amekuwa akitumika kama mchezaji wa akiba ambapo katika mechi dhidi ya Hull City na ile ya  Stoke City mchezaji huyo amliinga katika kipindi cha pili cha michezo hiyo. 

Mpaka sasa mchezaji huyo amefanikiwa kufunga goli moja tu tangu ajiunge na miamba hiyo ya Uingereza mwezi September mwaka huu hali inayompelekea  kuwa na wakati mgumu katika kikosi hicho.

Pia Van Gaal akithibitisha kuwa Rafael Da Silva ameshaanza mazoezi na timu hiyo tangu wiki iliyopita lakini hatowezacheza kwenye mchezo huo huku Phil Jones akitegemewa kuanza mazoezi na timu hiyo wiki ijayo.

Manchester United iliyopo nafasi ya tano ikiwa na pointi 25 katika michezo 14 iliyocheza inakwenda kucheza na Southampton iliyopo nafasi ya nne huku ikiwa na pointi 26 katika michezo 14 iliyocheza katika uwanja wa St Mary's huku ikitaka kushinda ilikujitengenezea mazingira mazuri ya kurudi kwenye timu nne za juu mara baada ya msimu uliopita kumaliza katika nafasi ya saba.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!