Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 August 2014
Monday, August 25, 2014

Mourinho bado anamuhitaji Fernando Torres



 Na Oscar Oscar Jr

Kumekuwa na hali ya sintofahamu juu ya kuondoka au kubaki kwa mshambuliaji wa Chelsea Fernando Torres ambaye anaonekana kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Jose Mourinho. Mechi mbili za ligi kuu ambazo Chelsea ameshacheza, Torres hakupewa kabasa nafasi.

Jose Mourinho amebainisha kuwa straika huyo raia wa hispania Fernando Torres, ana nafasi katika kikosi cha Chelsea licha ya mshambuliaji huyo kutotumika kwenye ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Leicester City mchezo uliofanyika siku ya Jumamosi. 

AC Milan wanatajwa kumfukuzia mshambuliaji huyo kwa kasi ili kuziba nafasi ya Mario Balotelli ambaye siku chache zilizopita amejiunga na klabu ya Liverpool. 

Torres hakuwepo hata kwenye benchi wakati Diego Costa akiendelea kuthibitisha kuwa yeye ndiye straika nambari moja na tayari ameshaifungia chelsea mabao mawili ndani ya mechi mbili alizoitumikia klabu hiyo yenye makazi yake jiji London.

Baadaye, Mourinho alisimama kidete na kusema kuwa anahitaji straika watatu ili kwenda sambamba na mahitaji husika kwenye mashindano mengi wanayoshiriki na kusema Torres atapata nafasi yake.

“Nataka straika watatu kikosini. Wakati mwingine nitacheza na wawili na moja wa akiba, wakati mwingine, mmoja atakuwa anatumikia marufuku au kuumia. Nataka (Torres) abaki hapa.”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!