NIONAVYO MIMI MTOTO WA TABORA:
SINA MASHAKA HATA KIDOGO NA SAFARI YA KASSEJA JANGWANI.
Na Oscar Oscar Jr
Golikipa
Juma Kasseja na mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa ni
aina ya wachezaji ambao mapenzi yao kwa Klabu za Karia koo huwa
yanawapa sana wasiwasi wapenzi wa timu hizo.Pamoja na kuwa Mrisho Ngassa
alichezea msimu uliopita klabu ya simba,wana msimbazi hawakumuamini na
sasa Juma kasseja anarejea Yanga kwa mara nyingine na ile dhana ya
mashabiki wa Yanga iko pale pale.
Mrisho
Ngassa na Juma Kasseja wanaponzwa na kitu kimoja tu,kuweka mapenzi yao
hadharani basi.Inasadikika kuwa Juma kasseja anaipenda sana timu ya
simba
na Mrisho Ngassa anaipenda sana timu ya Yanga.Kuipenda timu sio tatizo
hata kidogo,mshambuliaji wa klabu ya Arsenal,Theo Walcott tangu akiwa
mtoto mdogo ni shabiki mkubwa wa timu ya Liverpool na akikutana na
Liverpool huwa anawafunga magoli kama kawaida.
Juma Kasseja hakuongezwa mkataba na klabu ya Simba si kwa sababu ya umri wala kushuka kiwango,ni siasa zinazoendesha klabu ya Simba ndiyo chanzo cha yeye kutemwa na upande wa pili,Klabu ya Yanga nao wamemsajili kwa pesa nyingi sana pengine kuliko umri wake na kiwango chake ni kwa sababu za siasa hizo hizo zinazoendesha klabu ya Yanga!!
Anyway,mashabiki wanatakiwa kuelimishwa ili wajue kwamba,unapochezea YANGA sio lazima uwe shabiki wa timu hiyo.Hivi unadhani NIYONZIMA ni shabiki wa YANGA? unadhani TAMBWE ni shabiki wa SIMBA? Mwacheni kasseja akafanye kazi Yanga,kuipenda timu au kutokuipenda ni maisha yake binafsi.
0 comments:
Post a Comment