Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 January 2015
Wednesday, January 07, 2015

Wilfried Bony huyooo Manchester City


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Swansea, Wilfried Bony anakaribia kutua kwenye klabu ya Manchester City, taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema mshambuliaji huyo mwenye magoli 20 katika mwaka 2014 anatarajia kukamilisha dili la kujiunga na mabingwa hao watetezi siku za karibuni.

Bony aliondoka nchini Uingereza mapema wiki hii kwenda kujiunga na timu yake ya taifa nchini Abu Dhabi katika maandalizi ya michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika itayoanza tarehe 17 ya mwezi Januari.

Akiongea na waandishi wa habari akiwa kwenye uwanja wa ndege kabla ya kuondoka nchini Uingereza kuhusu majadiliano kati yake na Manchester City Bony alisema “yanaendelea, majadiliano yanaendelea. Kwasasa naenda kujiunga na timu yangu ya taifa na nafokasi huko”

Huku akionyesha hamu ya kutaka kujiunga na mabingwa hao wa EPL na kutaka kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya Bony aliendelea kusema “kwanini isiwe, kila mchezaji anataka kucheza kwenye ligi ya mabingwa na kombe la Dunia hivyo ni matamanio ya kila mchezaji”.

“Wakati ukipata nafasi mara nyingine hutokea na mara nyingine haitokei lakini nachukulia mambo taratibu, kwasasa ni timu ya taifa”

Wakala wa mshambuliaji naye akiongea na waandishi wa habari kuhusu mazungumzo yanayondelea na City alisema “mazungumzo yanaendelea na tunasubiri lakini tunatumaini mapema mambo yatakamilika, inaonekana kama yatakamilika, kwasasa ni City kulikuwa na mazungumzo na klabu zingine lakini kwasasa ni City.

Aliendela kusema “sio vizuri kuliongelea hili. Kuna mambo machache kuhusu fedha lakini natarajia mambo yataenda mbele katika siku chache zijazo, nina safiri nae kwenda Abu Dhabi hivyo tutaona nini kitatokea siku chache, siku chache”

Mpaka sasa Bony ambaye ameichezea Swansea michezo 70 na kuifungia magoli 34 toka aliposajiliwa mwaka 2013 akikamilisha usajili huo atakutana na changamoto kubwa toka kwa Sergio Aguero, Ediz Dzeko na Stevan Jovetic.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!