Searching...
Image and video hosting by TinyPic
12 November 2013
Tuesday, November 12, 2013

BAADA YA POLISI JAMII KUFANIKIWA,TUANZISHE SASA "SOKA JAMII"

NIONAVYO MIMI MTOTO WA TABORA:
 
BAADA YA POLISI JAMII KUFANIKIWA,TUANZISHE  SASA
"SOKA JAMII"

Na Oscar Oscar Jr

Jeshi la polisi nchini baada ya kuona ushiriki wa wananchi katika zoezi zima la kuwalinda wao na mali zao halifanikiwi vizuri,waliamua kuja na mchakato mpya ambao unakwenda kwa jina la "Polisi jamii" Mpango huu unamfanya kila mwananchi kufanya kazi ya askari polisi,kutoa taarifa,kulinda usalama wake na wa mwenzake,na kutoa ushirikiano pale ambapo polisi wanahitaji msaada wa raia.Mpango huu umezaa matunda. 

Timu ya Mbeya City Council ya jijini Mbeya wakati wakijiandaa kucheza na timu ya Tanzania Prisons "Green city derby" mwishoni mwa mzunguko wa kwanza wa Vodacom Premier league, wao na mashabiki walitembelea Hospital ya Mkoa wa Mbeya na kwenda kuwapa pole na misaada midogo midogo wakina mama wajawazito na waliokwisha jifungua.Waliporudi uwanjani,walimfunga Tanzania prisons 2-0.Unadhani wanahela sana??

Mashabiki wa Mbeya City Coucil wakiwa jijini Dar es alaam wakijiandaa na mechi yao dhidi ya Azam,walitembelea hospitali ya Amana na kufanya kile walichokifanya Mbeya.Kuwafariji wagonjwa na kuwapata misaada midogo midogo na waliporudi uwanjani,walipata sare ya 3-3 dhidi ya Azam fc! Unadhani wana Elimu sana??

Siku Mrisho Ngassa,Peter Michael,John Bocco na wengine wakitembelea shule za msingi na kuwanunulia wanafunzi kalamu tu,unadhani ni kwa sababu watakuwa na pesa sana?? 
Hao wanawake waliotembelewa na timu ya Mbeya City Council,unadhani nini kimebaki akilini mwao wanapowaona Mbeya City? Mtazamo wao kuhusu soka umebadilika kiasi gani??

Tunapotumia milango yote ya fahamu katika tukio moja,hujenga uelewa na kumbukumbu ya Kudumu.watoto wengi pengine hawaamini kama Juma Kasseja ni mtu,hawaamini kuhusu,Kipre Tchetche wala kuhusu Haruna Boban!

Siku moja wanafunzi wakipata nafasi ya kuwaona mastaa hawa shuleni kwao na angalau kuwashika mkono,inaweza kuibua hisia chanya kwao kuliko wanavyowaona kwenye TV! Mpira ni mchezo unaopendwa na watu wengi,tukitumia "soka jamii" tutafika mbali sana.
Anyway,binadamu anahitaji zaidi akili,pesa na elimu ni ziada tu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!