Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 January 2015
Saturday, January 10, 2015

Liverpool inazidi kuimarika, yakusanya pointi muhimu.


Na Oscar Oscar Jr

Harakati za Liverpool kuhakikisha kuwa wanamaliza kwenye moja kati ya nafasi nne za juu, zinashika kasi baada ya leo kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wachezaji 10 wa Sunderland. 

Sunderland walibakia 10 uwanjani baada ya Liam Bridcutt kupewa kadi nyekundu. Bao pekee lililofungwa na Lazar Markovic lilitosha kuwapatia Liverpool alama tatu muhimu.

Huu ni ushindi wa tatu kwenye michezi minne za ligi kuu za hivi karibuni na hii inawafanya Liverpool kuzidiwa alama nne pekee kuweza kutinga kwenye nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu. 

Liverpool sasa wametimiza alama 32 wakati nafasi ya nne ikishikiriwa na Southampton wenye alama 36 ambao wanajiandaa kucheza na Manchester United siku ya Jumapili.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!