Rais wa Barcelona atoa tamko kuhusu Lionel Messi.
Na John Oscar
Rais wa klabu ya Barcelona, Josep Bartomeu amelazimika kuja kufafanua baadhi ya mambo yanayohusu klabu hiyo baada mtafaruku wa hapa na pale uliopeleke kutimuliwa kwa mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.
Kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Real Sociedad huku Lionel Messi na Neymar wakianzia benchi na kitendo cha Lionel Messi kui-follow klabu ya Chelsea kwenye mtandao wa Instagram ni miongoni mwa habari zinazoitafuna Barcelona kwa sasa.
Akijibu hoja hizo Josep Bartomeu amedai kuwa, alimuondoa mkurugenzi wa ufundi kutokana na kushindwa kujiamini kwenye majukumu yake.
Kuhusu Messi, Rais huyo amedaikuwa Muajentina huyo bado ana mkataba na Barcelona na kinachoendelea hakika uhusiano wowote na mchezaji huyo kuhamia kwenye klabu ya Chelsea ingawa kama kuna klabu itatoa Pauni 196 na kukubaliana na mchezaji, watakuwa tayari kumuuza.
Alipoulizwa kitendo cha mchezaji huyo kui-follow akaunti ya Chelsea, Josep Bartomeu hakuna na jibu la kueleweka. Rais huyu amekanusha habari za kocha wa timu hiyo Luiz Enrique kupewa mechi mbili huku akitakiwa kushinda mechi hizo na kudai kuwa, Enrique bado ni kocha wa Barcelona na hakuna mashati yoyote kwenye utendaji wake wa kazi.
Rais amezungumzia pia dhamira yake ya kuitisha uchaguzi ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu huku akiweka dhamira yake ya kusimama na kutetea kiti chake lakini, kumekuwa na habari nyingine kuwa aliyekuwa Rais wa klabu hiyo Joan Laporta.
0 comments:
Post a Comment