Simba wamenifundisha kitu mchezo wa jana.
Samuel Samuel
0652464525
Nilipoitazama Simba SC ikipata ushindi mwembamba dhidi ya timu ya JKU , nilitafakari sana thamani ya klabu na fedha zinazotumika uwanjani dah! nikaishia kuhema kwa nguvu na kuendelea kumkazia macho kiungo Said Ndemla.
Moja ya viungo hatari zaidi ndani ya Msimbazi ambaye almanusura atue Azam FC usajili wa dirisha dogo mwaka jana. Sijui kiliwapata nini viongozi wa Simba na benchi lao la ufundi kutaka kudhihaki kazi ya mzawa huyo aliyeko timu ya taifa. Tuachane na kiungo huyo haikuwa nia yangu kumzungumzia kiungo huyo.
Baada ya kuisoma Simba jana kabla ya mechi na nilopoitazama Taifa Jang'ombe ambayo ni moja ya timu dhaifu sana katika mashindano hayo na isitoshe ilicheza mechi mfululizo , nikajua ikifika dakika ya 35 Simba itakuwa mbele kwa goli si chini ya 3!
Daah. Kulia kulikuwa na kiungo machachari Ramadhani Singano, kushoto mfalme wa mtani jembe Awadhi Juma wakati kiungo wa mbele alisimama Said Ndemla.
Twende kazi pale kati. Walisimama wachezaji wenye nguvu na kasi Maguli na Sserunkuma. Wakati beki za kulia na kushoto walikuwepo vijana wenye nguvu kusaidia mashambulizi ya pembeni. Tshabalala na Miraji. Langoni kinda mwenye kipaji Manyika Jr.
Kati chini Jonasi Mkude kama kiungo mkabaji akisaidiwa na walinzi wa kati Isihaka na Juud. Hivi inakuwaje dk 45 hupati hata goli la offside hapo? Ebooh Wacha niyatandikie zuria jekundu mawazo wangu kwa kile alichofanya kocha Goran kipindi cha pili.
Wakati kipindi cha pili kinaanza yalifanyika mabadiliko mmmh, jamaa yangu pembeni akaniuliza " Sam huyu anayeingia ndio nani?" Ilinichukua dakika tano kufikiria jibu sahihi katika swali lake. Mwisho wa siku nikamjibu ' mchezaji wa Simba' Jamaa alinitazama lakini hakutia neno.
Tukaendelea kuangalia mpira. Kijana yule ilimchukua dakika nne tu kufanya kile ambacho mashabiki wa Simba zaidi ya milioni nne nchi nzima walikuwa wanakisubiri.
Dk ya 49 alicheka na nyavu. Ndipo nilipomgeukia yule jamaa Yangu . " una muona yule golikipa ? Manyika Jr, yule winga wa kulia Singano. Geuka na kule kushoto kuna Juma Awadhi sawa? " akajibu nawaona.
Nikaendelea ... " yule kiungo mkabaji pale kati na beki wa kushoto wote hao wametoka alipotoka huyu aliyefunga hili goli" jamaa alinitazama kisha akaropoka " Uganda?!" Nilitaka kucheka ila nikamezea baada ya kuona Ibrahim Hajib akitupia goli la pili .
Wachezaji hao wote na yule kiungo mchezeshaji Said Ndemla wametoka walikotoka lakini wamenolewa na Simba B. Ni kama vile Simba inavuna kile ilichopanda. Ibrahim anatuambia thamani ya kujali soka la vijana na kutunza vikosi vyetu vya timu B.
Mchezaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheza kiungo cha chini, mbele , kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wa pembeni amefikisha ujumbe wa Simba SC kulea na kuthamini soka la vijana kuliko kutumia mamilioni ya fedha kusajili wakongwe toka nje ambao wanacheza kwa muda mfupi na hakuna msaada wowote kwa timu yetu ya Taifa.
0 comments:
Post a Comment