Tetesi za usajili wa Gunners.
Na John Oscar
Habari za Usajili zimeendelea na leo hii klabu ya Arsenal imehusishwa na wachezaji watatu huku kiasi cha Pauni 50M zikitajwa kufanikiwa usajili huyo.
Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Southampton, Morgan Schneiderlin ametajwa kuwindwa na Gunners huku gharama ya uhamisho wake ikitajwa kuwa Pauni 25M.
Mchezaji mwingine ambaye kocha Arsene Wenger ametajwa kumnyemelea, ni kiungo kutoka klabu ya Sporting Lisbon, William Carvalho.
Kiungo huyo amekuwa pia kwenye rada za Manchester United na Chelsea na kama Wenger akiamua kumpeleka Emirates, mchezaji huyo atamgharimu Pauni 20M.
Kwa upande mwingine, kocha Wenger ameonekana kutofurahia mwenendo wa safu yake ya Ulinzi na sasa amepania kumuongeza beki mwingine wa kati ili aje kucheza na Laurent Conscienly na kumpumzisha Per Mertasacker ambaye ameonekana kuyumba msimu huu.
Beki wa Saint-Etienne, Loic Perrin anatajwa kuwa njiani kuelekea Gunners na gharama yake ni Pauni 6M. Arsenal ambao wanakamata nafasi ya sita kwenye ligi kuu, watahitaji kupamabana hasa ukizingatia kuwa Tottenham, West Ham United na Southampton wanaonekana kuwa wapinzani wakuu msimu huu kwenye nafasi nne za juu.
0 comments:
Post a Comment