Sami Hyypia aachia Ngazi
Na Florence George
Aliyekuwa Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Finland pamoja na timu ya soka ya Liverpool ya Nchini Uingereza, Sami Hyypia amtengaza kuachia ngazi katika nafasi ya ukocha katika klabu ya Brighton inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza.
Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa timu hiyo Tony Bloom siku ya jumatatu mchana mara baada ya hapo awali Sami kupeleka barua ya kuomba kuacha kufundisha timu hiyo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa, Hyypia alikuwa akipata wakati mgumu tangu alipojiunga na timu hiyo majira ya joto mwaka huu japo kuwa timu ilikuwa inacheza vizuri huku matokeo yakibaki kuwa mabaya katika timu hiyo kitu kilichopelekea kuomba kuacha kuifundisha timu hiyo.
Bloom aliendelea kusema kuwa Hyypia ataendelea kukumbukwa na kuheshimiwa kwa yale mazuri zote aliyoifanyia timu hiyo ,huku akiamua kuachia ngazi kwa manufaa ya timu na klabu kwa ujumla.
Sami Hyypia alichukua nafasi hiyo mwezi wa sita mwaka huu na kusaini Mkataba wa miaka mitatu lakini matokeo mabaya ndio chanzo cha yeye kuondoka kwenye timu hiyo kwani ameshinda michezo mitatu kati ya 22 iliyocheza timu hiyo msimu huu.
Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspurs Tim Sherwood ndie anahusishwa na taarifa ya kuja kuchukua nafasi hiyo hata hivyo atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa kocha wa MK Dons Karl Robinson anayetajwa pia kuhitaji nafasi hiyo.
0 comments:
Post a Comment