Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 December 2014
Tuesday, December 30, 2014

Makocha wanne ndani ya mwaka mmoja!


Na Chikoti Cico

Kocha wa zamani wa Stoke City na Crystal Palace Tony Pulis anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa West Bromwich Albion akichukua nafasi ya Alan Irvine aliyefukuzwa kazi mapema wiki hii.

Taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema Pulis aliyetakiwa na timu ya Newcastle United ambayo kocha wake Alan Pardew ameamua kuondoka na kwenda kuifundisha Crystal Palace amegoma kwenda timu hiyo baada ya kupata wasiwasi kwamba mmiliki wa timu hiyo Mike Ashley na kiongozi wa kutafuta vipaji Graham Carr wataingilia kazi ya upangaji wa timu.

Hivyo baada ya kuikataa Newcastle Pulis kupitia washauri na mawakili wake walianzisha mazungumzo na timu ya West Brom na wamekubaliana kwamba kocha huyo mwenye miaka 56 ataanza kuifundisha timu hiyo baada ya maofisa wa West Brom kukubali kwamba Pulis ndiye atakuwa anahusika na mambo ya usajili kwenye timu hiyo.

Pulis anakuwa kocha wa nne kuifundisha timu ya West Brom ndani ya mwaka mmoja baada ya Steve Clarke, Pepe Mel na Alan Irvine wote kufukuzwa kazi kutokana na timu kuwa na mwenendo mbaya kwenye ligi kuu nchini Uingereza, Pulis anatarajiwa kuiongoza timu hiyo kwenye mchezo wa kombe la FA kwa raundi ya tatu dhidi ya Gateshead hapo Jumamosi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!