NIONAVYO MIMI PALE SANTIAGO BERNABEU.
Real Madrid kuna vitu vya msingi ambavyo vinawasumbua na wanataka kumleta Mtaliano Carlos Anceloti awasaidie baada ya Mourinho Kushindwa.
1.Utawala wa Barcelona
Hiki ni kitu kinachowasumbua sana Madrid awali waliamini kwamba Mourinho anaweza kazi hiyo lakini amechemsha.Alipigwa sana na Pep Gaudiola,afadhali hata kwa Tito Vilanova na Jordi Raura,Mourinho kapumua kidogo.
2.La masia Academy
Hii ni shule ya soka ambayo kwa miaka ya hivi karibuni imetoa vijana ambao wameisumbua Dunia,Xaiv,Iniesta na Messi ni baadhi tu.Real Madrid kama wafalme wa Hispania wanahitaji mtu wa kuwaendeshea academy kama hii na ndiyo maana,walimtaja wenger na sasa,Anceloti nadhani wamepatia.
3.Ubingwa wa 10 wa UCL
Hiki ni kitu ambacho Madrid wamekuwa wakingojea kwa muda sasa,kumleta Carlos Anceloti nadhani hawajakosea.Mtaliano huyu kalichukuwa kombe hilo kama kocha na kama mchezaji.Anambinu na anajua kuwaunganisha Bodi,wachezaji na mashabiki.
Trust me,Kama ancheloti atatua Real Madrid na kupewa muda kwenye utendaji wake,Madrid mpya itazaliwa.
Chelsea hakupewa muda ingawa aliwapa vikombe viwili na PSG kaibadilisha sana na kachukuwa Kombe.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.