Al ahly mabingwa kombe la shirikisho
Na Florence George
klabu ya soka ya Al ahly tokea nchini misri imefanikiwa kushinda kombe la shirikisho barani Afrika mara baada ya kushinda goli 1-0 dhidi ya Sewe Sport ya nchini Ivory Coast mchezo uliochezwa Cairo nchini Misri.
Al ahly iliingia uwanjani huku ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa goli 2-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa tarehe 29 november Abidjan nchini Ivoy Coast, hivyo ilikuwa inahitaji ushindi wa goli moja au zaidi ili waweze kuwa mabingwa wa kombe hilo.
Sewe Sport walitawala katika kipindi cha kwanza huku wakihitaki sare ya aina yoyote ile ili waweze kuwa mabingwa lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili na Al ahly kutawala mpira huku Emad Meteb akiibuka shujaa wa timu yake.
Mateb alibadilisha hali ya mchezo baada ya kufunga goli pekee katika dakika 15 za mwisho na kufanya matokeo yasomeke 2-2 hali iliyopelekea Al ahly kushinda kwa sheria ya goli la ugenini.
Al ahly ndio timu ya kwanza ya nchini Misri kushinda kombe hilo, pia ikiwa na kocha wa kigeni kutoka nchini hispania Juan Carlos Garrido.Ushindi huo umewafanya Al ahly kufikisha jumla ya makombe tisa iliyojikusanyia katika michuano mbalimbali barani Afrika, huku klabu bingwa Afrika wakichukua mara nane na kombe la shirikisho mara moja.
0 comments:
Post a Comment