Na Chikoti Cico
Kocha wa Manchester United Mdachi, Louis van Gaal achukizwa na utaratibu wa chama cha soka cha nchini Uingereza (FA) kwa kupanga mechi baada ya mechi kwenye siku za krismasi na mwaka mpya huku akisema ni utaratibu ambao unaharibu taswira ya ligi ya Uingereza maarufu kama “Barclays Premier League”.
Van Gaal ambaye wachezaji wake walionekana dhahiri kuchoka kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tottenham Hotspur uliochezwa siku ya Jumapili na mechi hiyo kuisha kwa matokeo ya sare ya 0-0 wakati huo huo United wanajiandaa na mchezo wa siku ya mwaka mpya dhidi ya Stoke City na mchezo mwingine wa kombe la FA siku ya Jumapili dhidi ya Yeovil.
Akiongea na waandishi wa habari Van Gaal alisema “Kila mtu anajua kwamba mwili hauwezi kupata nafuu ndani ya masaa 48 hivyo kuna sheria pale UEFA na FIFA kwamba huwezi kucheza michezo iliyokaribiana sana, sawa hilo nililisema, kisayansi limethibitishwa na hilo pia nililisema, kila mmoja analijua hilo ila pamoja na hilo inabidi tucheze”.
Alendelea kusema “ni utamaduni wa Uingereza, sina shida lakini sio nzuri kwa wachezaji, kwa afya ya wachezaji na ninalolisema sasa ni kwamba ni vizuri kwaajili ya mchezo kwasababu nafikiri kwamba FA pia mashabiki wanataka michezo inayovutia lakini haitokei, uliona kipidi cha pili pale Tottenham, uliona kipindi cha pili cha Chelsea dhidi ya Southampton, mpira haukuwa mzuri”
Wakati ligi za nchi mbalimbali kama Hispania na Ujerumani zikiwa mapumziko katika kipondi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka nchini Uingereza hali ni tofauti kwani bado ligi inacheza na mechi zimekuwa zikicheza katika tofauti ya siku mbili kitu ambacho kocha wa Manchester United Van Gaal hajakifurahia.
0 comments:
Post a Comment