Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 December 2014
Tuesday, December 30, 2014

Hali si shwari tena ndani ya Barcelona.


Na Chikoti Cico

Rufaa ya timu ya Barcelona ya nchini Hispania kwenye mahakama ya usuluhishi ya michezo (CAS) dhidi ya adhabu ya kufungiwa kufanya usajili kwenye madirisha mawili ya usajili na shirikisho la soka Duniani (FIFA) imekataliwa na mahakama hiyo.

Barcelona walipatikana na hatia ya kusajili wachezaji walioko chini ya umri unaotakiwa kutoka nje ya Hispania kitu ambacho kilisababisha FIFA wawafungie kufanya usajili kwa mwaka 2015 na baada ya kukata rufaa dhidi ya adhabu hiyo mahakama ya usuluhishi ya michezo CAS imeitupilia mbali rufaa hiyo.

Hukumu ya CAS iliyotolewa siku ya Jumanne ilisema “CAS imeondoa rufaa iliyokatwa na Barcelona FC dhidi ya FIFA kuhusu uamuzi uliotolewa na kamati ya rufaa ya FIFA hapo Agasti 19. 2014”.

“Jopo limegundua mahususi kwamba Barcelona FC walikiuka sheria kuhusu ulinzi wa watoto na usajili wa watoto wanaohudhuria shule za mpira, ipasavyo, uamuzi wa FIFA umehakikiwa inavyotakiwa na adhabu inabaki kuendelea”

Rufaa ya Barcelona kwa CAS ulilazimisha kuchelewa kwa adhabu ya kufungiwa kwa mara ya kwanza na kuruhusu timu hiyo kuwasajili Luis Suarez, Ivan Rakitic, Alen Halilovic na wengine wakati wa majira ya joto kwenye ya dirisha la usajili kwa mwaka 2014.

Hivyo uamuzi huo wa CAS ni wa mwisho kuhusu kufungiwa kwa Barcelona na adhabu ya kutokusajili mchezaji yeyote itaanza wakati wa dirisha dogo la usajili mapema mwezi wa kwanza na kipindi cha majira ya joto kwa mwaka 2015, Barcelona wataruhusiwa kusajili tena kuanzia Januari 2016 na pia kulipa faini ya karibu kiasi cha Euro 375,000.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!