Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 December 2014
Tuesday, December 30, 2014

Dau la Salumu Telela limepanda kwa sasa.



 Na Samuel Samuel

Tofauti kubwa niliyoiona juzi kati ya Athuman Idd na Salumu Telela ni namba za jezi. Chuji akiitumikia timu Yanga alikuwa akivaa jezi namba 20 ilihali sasa Telela anavaa jezi namba 2. 

Vijana wa kocha Joseph Omog timu ya Azam, walipakimbia kati kwa uwezo mkubwa aliouonesha Telela. Aliweza kuiunganisha timu huku akiitengeneza timu katika mifumo yote. 

Telela alihakikisha Yanga ina miliki mpira kwa pasi fupi fupi lakini aliiongoza timu kushambulia kwa pasi pembe zenye kasi na hata mipira mrefu. 

Telela akiwa katika ubora wake dakika ya 27 alitoa krosi nzuri ambayo ilitiwa kwenye kamba na Tambwe. Kpah Sherman ajilaumu kushindwa kuondoka na goli kwenye mechi ile. 

 Kila mara Telela alikuwa akimpa pasi murua na kuufanya uwanja mzima ulipuke kwa furaha. Maboss hawa hawa wa Yanga ndio waliompa thamani ya mamilioni ya pesa Frank Domayo sina Shaka baada ya muda mfupi, Salumu Telela hata sajiliwa kwa milioni 10 tena dau litapanda! 

Inaweza kuonekana kama ni mapema kumlinganisha mchezaji huyo na waliomtangulia, wafalme wa dimba kama Chuji na Domayo lakini anakila dalili za kuja kutatua tatizo la sehemu ya kiungo ambalo limekuwa linawatesa Yanga tangu kuanza kwa msimu huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!