Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 December 2014
Tuesday, December 30, 2014

Klabu ya soka ya Everton yapata pigo





Na Florence George


Klabu ya soka ya Everton ya Nchini Uingereza imepata pigo mara baada ya kocha wa klabu hiyo, Roberto Martinez kutangaza kuwa kipa namba moja wa timu hiyo, Tim Howard atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 aliumia katika kipindi cha kwanza mechi dhidi ya Stoke City siku ya ijumaa ambapo timu yake ilifungwa goli 1-0,na nafasi yake kuchukuliwa na Joel Robles,ambaye pia alicheza katika mechi dhidi ya Newcastle United jumapili iliyopita na Everton kupoteza mchezo huo kwa kufungwa 3-2.

Akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo dhidi ya Hull City siku ya Mwaka Mpya, kocha Martinez alisema kuwa Howard atakosekana katika timu hiyo kwa muda wa wiki tano hadi sita kutokana na majeraha aliyopata katika mechi hiyo.

Mchezaji huyo atakosekana katika michezo mbalimbali ya ligi kuu zikiwamo dhidi ya Hull City,Manchester City,West Bromwich Albion, Crystal Palace na Liverpool huku pia akikosa katika mchezo wa raundi ya tatu ya kombe la FA dhidi ya West Ham United.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!