Raisi wa Real Madrid aigomea Manchester United
Na Florence George
Raisi wa klabu ya soka ya Real Madrid, Florentino Perez ameendelea kusisitiza kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale kuwa hawezi kuuzwa kwenda timu yoyote ile japokuwa kumekuwa na taarifa kuwa Manchester United ya Nchini Uingereza imekuwa ikimuhitaji mcheaji huyo.
Manchester United imekuwa ikiripotiwa kumuhitaji mchezaji huyo huku ikimtengea kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kumsajili, ambaye alijiunga na miamba hiyo ya Hispania katika majira ya joto mwaka 2013 kwa kitita kilichoweka rekodi cha paundi 86 millioni.
Pia kumekuwa na taarifa kuwa Real Madrid inataka kubadilishana mchezaji huyo na goli kipa wa United David de Gea lakini Perez ameviambia vyombo vya habari vya Dubai kuwa Mabingwa hao wa ulaya hawana mpango wowote ule wa kumuuza mshambuliaji huyo.
Aliendelea kusisitiza kuwa hawajapokea ofa yoyote kutoka Manchester United au klabu nyingine na hawako tayari kusikiliza ofa yoyote ile hata kama watakuwa wametoa kiasi kikubwa cha pesa.
0 comments:
Post a Comment