Semi Khedira haendi kokote
Na Oscar Oscar Jr
Semi Khedira ni kiungo ambaye ameingia kwenye tetesi za kuihama klabu ya Real Madrid kwa muda mrefu sana na hii inatokana na wababe hao wa Ulaya kuwasajili Toni Kroos na James Rodriquez huku Luke Modrid naye akiendelea kufanya vizuri.
Khedira hakuwepo nchini Hispania kwenye mechi ya mkondo wa pili wa Supa Copa dhidi ya Atletico Madrid Ijumaa iliyopita huku akiripotiwa kwenda kumtazama ndugu yake aitwaye Rani aliyekuwa akicheze kikosi cha daraja la pili Ujerumani, RB Leipzig.
Kiungo huo ambaye alionekana kufanya vizuri alipokuwa anacheza na kiungo mwenzie Xaib Alonso alipoulizwa juu ya mustakabali wake pale Bernabeu alisema chochote kinaweza kutokea kabla ya Agosti 31.
Arsenal, Chelsea, Fiorentina na Bayern Munich wamekuwa wakifuatilia hali yake wakinuia kumsaini ikiwa ataondoka Real. Habari kutoka Hispania zimesema kuwa kocha Ancelloti bado anamuhitaji kiungo huyo na haendi kokote.
0 comments:
Post a Comment