Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 December 2014
Tuesday, December 30, 2014

Manchester United yaongeza majembe.






Na Florence George

Wachezaji wa timu ya soka ya Manchester United ya nchini Uingereza, Ander Herrera na Adnan Januzaj wamerejea katika mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na Mchezo dhidi ya klabu ya soka ya Stoke City siku ya Mwaka Mpya na hii ni kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo, Louis Van Gaal.

Manchester United inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu nchini humo imeshinda michezo saba kati ya tisa iliyocheza hivi karibuni,Alhamisi hii itasafiri kuwafata Stoke City katika muendelezo wa mechi za ligi kuu nchini humo.


Akiongea katika mkutano na waandishi wa Habari, Van Gaal alisema kuwa Herrera ameanza mazoezi siku ya jumanne huku Januzaj akiwa tayari ameshahudhuria mazoezi kwa vipindi viwili.

Aliendelea kusema kuwa wachezaji hao wanatakiwa kufanya mazoezi ili waweze kurudi katika ubora wao na kuweza kusaidia timu hiyo yenye maskani yake Old Trafford.

Pia Van Gaal amekiri kuwa na wakati mgumu katika kipindi hichi cha sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya ambapo jumapili wiki hii ilishuhudiwa kocha huyo akichezesha kikosi  dhidi ya Tottenham Hotspur ambayo kilichocheza dhidi ya Newcastle United siku ya ijumaa.


Manchester United imekuwa na tatizo la majeruhi huku ikishuhudiwa wachezaji Rafael, Chris Smalling na Luke Shaw wakipona majeraha yao huku Daley Blind, Marouane Fellaini,Marcos Rojo na Angel Di Maria wakiwa bado hawajapona majeraha yao hivyo kuendelea kuwa nje ya uwanja .

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!