Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 December 2014
Tuesday, December 23, 2014

Ferguson amwonea wivu Mourinho.


Na Chikoti Cico

Kocha wa zamani wa timu ya Manchester United Sir Alex Ferguson amzungumzia kocha wa Chelsea Jose Mourinho wakati akihojiwa kwenye studio za BT Sport, kwenye mahojiano hayo Ferguson amemsifia Mourinho huku akionyeshwa kufurahishwa na kazi alizofanya kocha huyo mzaliwa wa Ureno kwenye timu mbalimbali.

Kwenye mahojiano hayo Ferguson akimzungumzia Mourinho alisema “Sio haki kwakweli, ana mwonekano mzuri, ana nywele kidogo kama za George Clooney kwasasa lakini nafikiri ni mfano mzuri, anaweza kuzungumza lugha tano ama vyovyote anavyoweza.

Alikwenda na kuwa mtafsiri wa Bobby Robson, akamfwata Barcelona akafanya kazi chini ya Louis Van Gaal, anajifunza wakati wote”

Ferguson ambaye aliifundisha timu ya Manchester United kwa miaka 27 akiendelea kumzungumzia Mourinho alisema “ana maazimio, anataka kuwa kocha, hakuwahi kucheza mpira, mathalani niambie marahisi wangapi watampa kazi meneja ambaye hajawahi kucheza mpira? Hakuna. Lakini amefanya”.

“Halafu ameenda na kufundisha timu ndogo Ureno, halafu akaenda Porto na kushinda kombe la ligi, akashinda kombe la UEFA, akashinda kombe la Ulaya akaenda Chelsea akashinda kombe la ligi. Akaenda Inter Milan. Huo ni mfano kwa yeyote anayetaka kufanya vizuri, hutakiwi kuacha vigingi viingilie njia yako kama unataka kufika pale”

Wakati huo huo Mourinho ameiongoza Chelsea kuongoza ligi mpaka wakati wa Krismasi huku wakiwa na alama 42 kwenye msimamo wa ligi wakifuatiwa na Manchester City wenye alama 39 lakini pia kocha huyo ameiongoza Chelsea kucheza michezo 17 ya ligi huku wakipoteza mchezo mmoja tu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!