Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 December 2014
Tuesday, December 23, 2014

Wilshere si kitu mbele ya Fabregas.


Na Chikoti Cico

Inawezekana ikawa ni takwimu mbaya kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kuiona ama hata kuisikia kutoka kwa Cesc Fabregas lakini ndivyo ukweli wa mambo ulivyo hasa baada ya kukataa kumsajili mchezaji huyo wakati akitokea timu ya Barcelona kwenye kipindi cha usajili kilichopita.

Baada ya kuacha kumsajili Fabregas, Wenger alipoulizwa kama chaguo la kwanza la Fabregas ni kurejea Arsenal alijibu “hakika ndiyo, lakini alipoondoka tulimnunua Mesut Ozil, tuna Santi Carzola, Jack Wilshere na hatukuwa na haja ya kununua mchezaji wa kushambulia”

Lakini majibu hayo ya Wenger yanaonekana kwenda kinyume na takwimu bora za Fabregas toka atue Chelsea, mpaka sasa kiungo huyo kutoka Hispania amehusika kwenye magoli 14 ya Chelsea katika michezo 16 aliyocheza, huku akifunga magoli mawili na kutoa pasi za mwisho (assist) 12.

Kwa “assist” hizo 12 katika mechi 16 takwimu zinaonyesha kwamba Fabregas amemzidi Jack ilshere kwa assist katika mechi zake zote alizoichezea timu ya Arsenal.

katika michezo 95 aliyoichezea Arsenal Wilshere amepiga “assist” 11 tu hivyo kuzidiwa na Fabregas ambaye amecheza mechi chache sana ukilinganisha na Wilshere.

Wakati huo huo Wilshere ambaye ana miaka 22 mpaka sasa amcheza mechi tisa tu toka kuanza kwa msimu huu kabla ya kuumia mwishoni mwa mwezi Novemba na hivyo akitarajiwa kukaa nje kwa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye mguu wake wa kushoto.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!