Na Florence George
klabu ya soka ya Fc Barcelona imefanikiwa kurudi katika nafasi pili katika ligi kuu nchini Hispania baada ya kuifunga timu ya soka ya Espanyol magoli 5-1 mchezo uliopigwa katika dimba la camp nou.
katika mchezo huo ambao Fc Barcelona ilitawala kwa asilimia 79 ililazimika kutoka nyuma mara baada ya Sergio Garcia kuifungia Espanyol goli la kuongoza katika dakika ya 13 tu ya mchezo huo,
nyota wa klabu hiyo kutoka Argentina Lionel Messi alifanikiwa kuisawazishia timu yake katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza hivyo timu kwenda mapumziko zikiwa zimefungana 1-1.
Fc Barcelona ilirudi kwa kasi katika kipindi cha pili na ilifanikiwa kupata magoli mengine manne yaliyofungwa na Pedro,Gerrard Pique huku Messi akifunga wawili na kukamilisha hat trick yake ya 21 katika ligi kuu nchini Hispania.
kwa matokeo hayo yameifanya Fc Barcelona kushika nafasi ya pili ikifikisha pointi 34 katika mechi 14 iliycheza nyuma na vinara timu ya Real Madrid yenye pointi 36 katika michezo 14 huku Athletico Madrid ikishuka hadi nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 32 ambayo pia imecheza mechi 14
sasa Barcelona wanajipanga kupambana na klabu ngumu ya PSG ya nchini Ufaransa katika ligi ya klabu bingwa barani ulaya,mechi itakayochezwa katika dimba la Camp Nou siku ya Jumatano usiku.
0 comments:
Post a Comment