Mourinho apata kiwewe mara baada ya kufungwa na Newcastle United
Na Florence George
Mara baada ya kucheza michezo 14 katika ligi kuu nchini Uingereza bila kufungwa hatimaye klabu ya soka ya Chelsea siku ya jumamosi katika dimba la St James Park ilikubali kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa vijana wa Alan Pardew Newcastle United.
katika mchezo huo newcastle walionekana wakicheza kwa tahadhali kubwa na kuwapa uhuru vijana wa Chelsea kucheza mpira pande zote za uwanja,hadi kipindi cha kwanza kinamalizika kulikuwa hakuna timu ambayo iliyokuwa imeona lango la mwenzake.
kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kocha Alan Pardew alimuingia mshambuliaji wa senegal Papiss Cisse aliyekuja kufunga magoli mawili ya Newcastle kabla ya mkongwe Didier Drogba kuifungia timu yake goli la kufutia machozi dakika ya 83,hivyo hadi refa anapuliza filimbi ya mwisho matokeo yalibaki kuwa hivyo.
mara baada ya mechi hiyo kocha wa Chelsea Jose Mourinho aliwalalamikia vijana waliokuwa wanaokota mipira katika mechi hiyo kuwa ndio chanzo cha timu yake kupoteza mechi hiyo kwani walikuwa wanachelewesha mipira na muda mwingine walikuwa wanarusha mipira zaidi ya mmoja uwanjani .
kwa matokeo hayo Chelsea imeendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 36 katika michezo 15,ikifuatiwa na Manchester City yenye alama 33 iliyocheza michezo 15 pia.
0 comments:
Post a Comment