Messi apiga Hat trick afikisha magoli 402.
Na Florence George
Mara baada ya kuifunga timu ya soka ya Espanyol magoli 5-1 siku ya jumapili, klabu ya soka ya Fc Barcelona imesogea hadi nafasi ya pili katika msimamo wa liku kuu nchini Hispania kwa kufikisha jumla ya pointi 34 katika michezo 14 iliyocheza msimu huu nyuma ya vinara Real Madrid yenye pointi 36 katika michezo 14 iliyocheza msimu huu pia.
katika mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Camp Nou ilishuhudiwa mchezaji bora wa dunia mara nne mfululizo toka mwaka 2009-2012 Lionel Messi akifunga hat trick yake ya 21 tangu alipoanza kuichezea timu hiyo katika ligi kuu nchini Hispania.
Messi alifunga magoli hayo, siku moja mara baada ya mpinzani wake wa karibu Cristiano Ronaldo wa Real Madrid kufunga hat trick dhidi ya Celta Vigo na kumfanya awe mchezaji aliyefunga hat trick nyingi (23)kuliko mchezaji yeyote katika ligi hiyo.
Messi ambaye anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa la liga pamoja na ligi ya mabingwa barani ulaya ,pia alifanikiwa kufikisha jumla ya magoli 402 tangu alipoanza kuichezea klabu yake hiyo katika mashindano mbalimbali na ile ya kirafiki.
kwa sasa Messi pamoja na timu nzima ya Barcelona wanajiandaa kuikabili timu ngumu ya PSG kutoka nchini Ufaransa katika mechi ya mwisho hatua ya makundi mechi itakayochezwa siku ya Jumatano usiku katika dimba la Camp NOU.
0 comments:
Post a Comment