Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 December 2014
Tuesday, December 30, 2014

Papiss Cisse aangukiwa na rungu la FA





Na Florence George

Mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal na klabu ya soka ya Newcastle United Papiss Cisse amekumbwa na adhabu ya kufungiwa mechi tatu na chama cha soka Nchini Uingereza FA mara baada ya kumpiga kiwiko Mchezaji wa timu ya Everton Seamus Coleman katika mechi ya ligi kuu nchini humo siku ya jumapili.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alimpiga kiwiko beki huyo katika ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Everton huku refa wa mechi hiyo Craig Pawson akishindwa kuona tukio hilo.

Taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa Newcastle United  ilielezea kuwa Cisse amekubali kuhusika katika tukio hilo huku akikubali adhabu hiyo kutoka chama cha soka Nchini humo.

Sasa mchezaji huyo atakosa mechi dhidi ya Burnley siku ya mwaka mpya ,dhidi ya  Leicester city tarehe 3 january katika kombe la Fa huku pia atakosa mechi dhidi ya Chelsea tarehe 10 january.

Hata hivyo mchezaji huyo alikuwa akitegemewa kukosa michezo miwili dhidi ya Leicester na Chelsea kutokana na kwenda kuiwakilisha nchi yake katika mashindano ya mataifa huru ya Africa huko Equatorial Guinea.

Cisse hadi sasa ameshafunga magoli tisa msimu huu huku akifunga magoli matano katika michezo sita ya hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!