Searching...
Image and video hosting by TinyPic
8 November 2014
Saturday, November 08, 2014

Brendan Rodgers sasa amechanganyikiwa.


Na Chikoti Cico

Baada ya mechi ya ligi kuu nchini Uingereza kati ya Liverpool dhidi ya Chelsea mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Anfield kuisha na timu ya Chelsea kushinda kwa magoli 2-1, kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amlalamikia mwamuzi wa mchezo huo Anthony Taylor kwa kuinyima timu yake penati.

Liverpool waliokuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Emre Can kwenye dakika ya tisa baada ya shuti kali la Can kumgonga Cahill na kujaa wavuni, kwenye dakika ya 14 Garry Cahill aliisawazishia Chelsea na dakika ya 67 Diego Costa aliipatia Chelsea goli la ushindi huku likiwa ni goli lake la kumi kwenye msimu huu wa ligi.

Kocha wa Liverpool baada ya matokeo hayo alimlalakia mwamuzi wa mchezo huo Taylor kwa kuuinyima Liverpool penati baada ya mpira uliopigwa na Steven Gerrard kuonekana kuzuiliwa kwa mkono na beki wa Chelsea Garry Cahill.

Kocha huyo akiongea na waandishi wa habari alisema “ Teknolojia kuja kwenye mchezo imekuwa ni vizuri, wakati mwingine itaenda upande wako na wakati mwingine itafanya kazi kinyume chako, inaumiza sana kwetu kwamba kulikuwa na maamuzi makubwa kwenye mchezo na hatukupata”

“Ilikuwa wazi ameshika na tulitakiwa kupata, kama tulikuwa hatupati magoli kwenye mchezo wa kawaida tulitakiwa kupata goli kwenye mpira wa penati, mwamuzi aliona wazi lakini labda alihitaji msaada toka kwa mshika kibendera”

Kwa matokeo hayo inamaanisha Liverpool amepoteza michezo mitatu ndani ya wiki moja hii ni baada ya kufungwa na Newcastle wikendi iliyopita na baadaye kufungwa na Real Madrid kwenye mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya na Chelsea siku ya Jumamosi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!