Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Paul Scholes ametoa
wito kwa mabingwa wa Uingereza ambao wamekuwa wakihangaika wasimteme
meneja David Moyes licha ya kichapo kingine cha aibu.
Wiki moja tu baada ya kushindwa 3-0 nyumbani na mahasimu wao wa jadi
Liverpool, United walilazwa kwa mabao sawa kwenye debi ya Manchester nyumbani
kwao Old Trafford Jumanne.
Edin Dzeko alifungia Manchester City la kwanza sekunde ya 43 na
straika huyo wa Bosnian akaongeza jingine mapema kipindi cha pili kabla
ya Yaya Toure kukamilisha kichapo hicho kwa bao la tatu dakika ya 90.Kichapo hicho kiliwaacha United wakiwa nambari saba kwenye ligi na alama 12 nyuma ya Arsenal walio nambari nne.
Matokeo hayo yameacha mashabiki wakiwa na mshangao, kwamba kikosi kile kile
kilichoshinda ligi msimu uliopita na meneja wa zamani Alex Ferguson
kabla ya kustaafu, kimekuwa hakijiwezi hivyo dhidi ya timu za Uingereza
kikiwa mikononi mwa raia huyo wa Scotland ambaye alichaguliwa na Fergie.
Lakini Scholes alisema kumlaumu meneja huyo wa zamani wa Everton
litakuwa kosa, akisema United wanafaa kumuunga mkono meneja huyo zaidi
soko litakapofunguliwa kuliko walivyofanya kipindi kifupi ambacho Moyes
amekuwa Old Trafford.
"Lazima msimame naye. Alinunua wachezaji kadha ambao hawajafanikiwa
lakini majira ya joto atahitaji usaidizi zaidi, hakuna shaka kuhusu
hilo,” Scholes aliambia Sky Sports Jumanne.
"Je aliungwa mkono ilivyotakikana majira ya joto yaliyopita? Sina
uhakika kuhusu hilo, lakini majira yajayo lazima aungwe mkono na
nafikiri kwamba anajua anahitaji wachezaji,” akaongeza mchezaji huyo wa
zamani wa kimataifa wa Uingereza.
Nemanja Vidic anatarajiwa kuwaacha na kujiunga na Inter Milan mwisho
wa msimu huku Rio Ferdinand na Patrice Evra wakiwa kwenye darubini.
Scholes alisema lazima Moyes aangazie kuimarisha safu ya ulinzi ya United, ingawa pia kumekuwepo na wasiwasi kuhusu safu ya kati.“Kwangu, inaonekana kuna ameneo kadha ambayo yanahitaji kuangazia,”
Scholes, ambaye hatimaye alistaafu msimu uliopita, alisema.
"Sehemu ya kati ya unaweza kusema wamekuwa wakiangazia
hilo kwa miaka kadha sasa na labda hawajapata jawabu mwafaka.
“Ninadhani ulinzi pia, ukizingatia kwamba Vidic anaenda – ni kama
Rio na Evra pia wataenda, mabeki watatu kati ya wanne wako wanaenda –
hiyo ni sehemu jingine ambayo anafaa kuangalia.
"Kwenda mbele, wako sawa. Lakini labda ni safu ya kati na ulinzi ambapo (Moyes) anafaa kuangazia.”
26 March 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment