Hazard kutua Real Madrid
Na Oscar Oscar Jr
Mambo yanaweza kuwa mabaya hasa kwa mashabiki wa timu wa Chelsea ambao wamekuwa wakinufaika sana na mchango mkubwa unaotolewa na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Eden Hazard ambaye ameanza kuhusishwa na kujiunga na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.
Real Madrid ni klabu ambayo imekuwa na utamaduni wa kukusanya wachezaji mahiri kutoka kwenye kila pembe ya Dunia na hivi karibuni, wameweza kuwanunu Gareth Bale, Toni Kross na James Rodriquez huku wakiruhu kuondoka kwa wachezaji Mesut Ozil, Angel Di Maria na Xaib Alonso.
Gareth Bale ameripotiwa kuwa kwenye sintofahamu kutokana na kuwa majeruhi kwa muda mrefu huku kiungo wa kihispania, Isco akionekana kuziba nafasi yake kutokana na kucheza vizuri kwenye mechi za La Liga na klabu bingwa Ulaya.
Gareth Bale ni mchezaji anayependwa sana na kocha wa Manchester United, Loius Van Gaal na tayari kuna taarifa kuwa, winga huyo atauzwa kwenda Old Trafford huku wababe hao wa Ulaya, wakitaka kumuongeza mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard.
Real wamepanga kumuuza Bale kwa Pauni 90M na wanajiandaa kutumia kitita hicho kuwashawishi Chelsea kumuachia Eden Hazard. Manchester United kwa muda mrefu sana wamekuwa wakihangaika ama kumrudisha Christiano Ronaldo au kumleta Gareth Bale lakini vyote havikuwezekana.
Hii inaweza kuwa fursa nyingine kwao ya kumpata moja ya wachezaji waliowahitaji kwa muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment