Na Rossa Kabwine
Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers amesisitiza kuwa haitaji kumuangalia Mario Balotelli kwa ukaribu zaidi ambaye walipishana na Jonjo Shelvey katika mechi ya kombe la ligi.
Rodgers alisisitiza kuwa, haitaji kumlinda Mario Balotelli dhidi ya wachezaji wengine katika ligi ya Uingreza kufuatia kutaka kupigana na kiungo wa Swansea City, Jonjo Shelvey.
Balotelli aligongana na kiungo huyo wa Swansea katika mchezo ulio zikutanisha timu hizo mbili kuwania nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la ligi Jumatano ya wiki hii.
Katika mechi hiyo, Liverpool walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mchezo ukipigwa kwenye dimba la Anfield. Balotelli alifunga bao la kusawazisha akitokea benchi kabla ya beki wa kati wa timu hiyo, Dejan Lovren kufunga bao la pili na la ushindi.
Brendan Rodgers alisema “ Sihitaji kumlinda Mario, yupo sawa na hakuna shaka” Kocha huyo aliwaambia waandishi wa habari. Kufuatia kauli ya Rodgers, Balotelli inaelekea atacheza mechi dhidi ya Newcastle mchezo utakaopigwa weekend hii.
Newcastle ambao waliifunga machester City 2-0 ugenini kwenye mechi ya Capital One Cup na ushindi wa 2-1 walipata kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tottenhan Hotspurs, unatazamwa kama ujio mpya wa mafanikio kwa kocha Alan Pardew.
Balotelli ataendelea kutafuta goli lake la kwanza la ligi kuu ya Uingreza kwa klabu yake ya Liverpool ingawa, watakuwa bila ya mshambuliaji wao Daniel Sturridge ambaye bado anasumbuliwa na maumivu ya goti.
Rodgers alithibitisha kuwa, Sturridge hatokuwa fiti kuelekea mechi hiyo na nafasi yake, itachukuliwa na Borin. Pia, kuna taarifa za beki wa kushoto, Jose Enrique kuikosa mechi hiyo dhidi ya timu yake ya zamani ya Newcastle United.
0 comments:
Post a Comment