Na Chikoti Cico
Usiku
wa Ligi ya mabingwa wa Ulaya unarejea Jumanne na jumatano ya wiki hii
na moja ya mechi zitakazopigwa siku ya Jumanne ni kati ya CSKA Moscow
dhidi ya Manchester City mechi itakayopigwa jijini Moscow kwenye uwanja
wa Arena Khimki pia
Msimu wa 2013/2014 timu hizi mbili zilikutana tena na Manchester City iliibuka kidedea kwa mechi zote mbili za nyumbani na ugenini huku ikishinda kwa magoli 2-1 ugenini na kushinda nyumbani kwa magoli 5-1.
Mechi hiyo itachezwa bila ya mashabiki baada ya UEFA kuwaadhibu CSK Moscow kwa kushindwa kuwadhibiti mashabiki wao ambao walihusika katika kuonyesha vitendo vya kibaguzi kwenye mechi dhidi ya Roma.
CSKA Moscow iliyopo mkiani kwenye kundi E baada ya kupoteza mechi zake mbili za awali dhidi ya Bayern Munich na Roma.
Wataingia kwenye mechi dhidi ya Manchester City wakitafuta ushindi wao wa kwanza lakini pia wanatarajiwa kuwakosa Alan Dzagoev na Pontus Wernbloom wambao wanatumikia adhabu huku wakiendelea kuwakosa Rasmus Elm, Vitinho na Kirill Panchenko ambao ni majeruhi kwa muda mrefu.
Manchester City watatakiwa kuwa makini na kumchunga mshambuliaji wa Moscow Mnaijeria Ahmed Musa ambaye mpaka sasa ana magoli matano kati ya mechi 10 alizocheza kwenye ligi kuu nchini Urusi .
Kikosi cha kocha Leonid Viktorovich Slutsky wa Moscow kinachotarajiwa kuanza: Akinfeev; Schennikov, Ignashevich, Berezutski, Fernandes; Natcho, Eremenko, Milanov, Tosic, Musa; Doumbia.
Manchester City inayoshika nafasi ya tatu kwenye kundi E nyuma ya Roma wenye alama nne na Bayern Munich wenye alama sita italazimika kupigana kufa na kupona kushinda dhidi ya Moscow ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuvuka kwa hatua ya 16 bora hasa baada ya kufungwa na Bayern Munich na kutoka sare na Roma kwa mechi mbili za mwanzo kwenye kundi E.
Kocha Manuel Pellegrini anatarajiwa kuwakosa viungo Frank Lampard ambaye aliumia kwenye mechi ya ligi dhidi ya Tottenham Hotspur na Samir Nasri ambaye ni majeruhi wa muda mrefu.
Beki Eliaquim Mangala ambaye hakucheza dhidi ya Spurs kutokana na kuwa majeruhi anatarajiwa kuwepo kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya CSKA Moscow.
CSKA Moscow watatakiwa kumchunga sana mshambualji wa Manchester City Sergio Aguero ambaye mpaka sasa ana magoli tisa kati ya mechi nane kwenye ligi kuu ya Uingereza huku manne kati yao akiyafunga dhidi ya Spurs siku ya Jumamosi.
Kikosi cha Man City kinachotarajiwa kuanza: Hart; Zabaleta, Kompany, Mangala, Clichy; Milner, Fernando, Toure, Milner; Aguero, Dzeko.

0 comments:
Post a Comment