Mchezaji afariki dunia akishangilia goli alilofunga.
Na Oscar Oscar Jr
Habari za kusikitisha zimelikumba soka la nchini India baada ya jumapili ya jana kuripotiwa taarifa za kupoteza maisha kwa mchezaji wakati akishangilia goli alilofunga.
Siku ya jumanne ya wiki iliyopita kulikuwa na mchezo kati ya Bethlehem Vengthlang vs Chanmari West fc ambao ulimalizika kwa Chanmari kuibuka na ushindi wa magoli 3-2.
Biaksangzuala ni mchezaji wa Chanmari West na alifunga bao lake kwenye dakika ya 62 ya mchezo huo na katika kushangilia goli hilo, alijikuta kwenye matatizo makubwa yaliyopelekea kifo chake.
Inadaiwa kuwa mchezaji huyo, alishangilia goli lake kwa kubinuka sarakasi (kinyume nyume) na kwa bahati mbaya, alijikuta akiangukia kichwa.
Baada ya tukio hilo, Biaksangzuala alikimbizwa hospitali iliyoko karibu na uwanja uliokuwa ukitumika kwenye pambano hilo na baada ya uchunguzi kufanywa, iligundulika kuwa amevunjika uti wa mgongo.
Aliendelea kupatiwa matibabu kwa muda wa siku tano na Jumapili ya jana, taarifa ilitolewa kuhusu mchezaji huyo kupoteza maisha. Ripoti imeendelea kueleza kuwa, mchezaji huyo alitaka kuruka sarakasi kama mbavyo mfungaji bora wa muda wote wa kombe la Dunia, Mrejemanu Miloslav Klose hufanya anapokuwa amefunga.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa 101greatgoals.com
R.I.P Biaksangzuala
0 comments:
Post a Comment