Na Chikoti Cico
Ligi
ya mabingwa Ulaya mzunguko wa kwanza kwenye hatua ya makundi itaendelea
tena kwa mechi kati ya Chelsea dhidi ya Maribor, mechi ambayo itapigwa
kwenye uwanja wa Stamford Bridge. Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu
hizi mbili kukutana kwenye michuano ya UEFA.
Chelsea inayoongoza kundi G ikiwa na alama nne baada ya kutoka sare na Schalke 04 na kuifunga Sporting Lisbon itahitaji kushinda mechi hiyo ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuongoza kundi na pia kuvuka kwenda kwenye hatua ya mtoano.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho anatarajia kumkosa Diego Costa ambaye bado anasumbuliwa na misuli hivyo Locy Remy ama Didier Drogba mmojawapo ataweza kuanza dhidi ya Maribor kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Chelsea huku Ramirez na Schurrle wakiwa bado kwenye hatihati ya kuwepo kwenye mchezo huo baada ya kuwa nje kwa zaidi ya wiki moja kutokana na kuwa majeruhi.
Kikosi cha Chelsea kitakachoweza kuanza kinaweza kuwa hivi:
Courtois; Luis, Cahill, Terry, Ivanovic; Matic, Fabregas; Schurrle, Hazard, Salah, Drogba
Timu ya Maribor kutoka Slovenia ingawa sio maarufu kwenye michuano ya UEFA lakini imeonakena sio timu ya kubeza kwani mpaka sasa wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi G.
Baada ya kujikusanyia alama mbili kwa kutoka sare dhidi ya Schalke 04 na Sporting Lisbon katika mechi ambazo waliingia kama “under dogs” huku wakipewa nafasi ndogo ya kushinda ukiachilia kupata sare.
Rekodi zinaonyesha timu ya Maribor inayofundishwa na kocha Ante Šimundža wana rekodi mbaya dhidi ya timu kutoka Uingereza kwani katika michezo tisa waliyocheza dhidi ya timu kutoka Uingereza kwenye michuano ya Ulaya, wamepoteza michezo sita, wametoka sare michezo miwili na kushinda mchezo mmoja dhidi ya Wigan Athletic.
Kikosi cha Maribor kitakachoweza kuanza kinaweza kuwa hivi:
Handanovic; Viler, Suler, Rajcevic, Mejac; Bohar, Mertelj, Filipovic, Vrsic; Tavares, Ibraimi

0 comments:
Post a Comment