Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 October 2014
Monday, October 20, 2014

Manchester United wanautaka ubingwa wa EPL.


Na Oscar Oscar Jr

Kocha mkuu wa Manchester United Loius Van Gaal, ameibuka na kudai kuwa Man United endapo itapata ushindi dhidi ya timu ya West Bromwich Albion usiku wa leo, watakuwa wamerudi rasmi kwenye mbio za kupigania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza ambapo mpaka sasa, Chelsea wanaongoza ligi hiyo.

Kocha huyo amehusisha ndoto hizo na kile amabacho alikifanya akiwa na klabu ya Bayern Munich ambao walisafiri na kwenda kupata ushindi wa bao 4-1 dhdi ya Juventus mwaka 2009 kwenye mchezo wa Uefa na baadae, wakafika fainal na kufungwa na Inter Millan. Pamoja na kupoteza fainal, Bayern walishinda taji la Ujerumani.

Chelsea, Arsena, Liverpool na Manchester City wako kwenye michuano ya Uefa huku Man United wakiwa nje na pia, wametolewa kwenye michuano ya Capital One Cup. Van Gaal ana amini kuwa hali hiyo ni faida kubwa kwa timu yake kupigania ubingwa.

Katika mahojiano ya leo, bado timu hiyo itaendelea kukosa huduma za wachezaji wake Lingard, Paddy Mcair, Jonny Evans na Antonio Valencia. 

Loius Van Gaal anaelekea kuwa Man United walikuwa bora sana kwenye mechi dhidi ya Everton kwa dakika 60 pekee na leo anatarajia, vijana wake watakuwa imara kwa dakika zote 90.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!