Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 October 2014
Friday, October 31, 2014

Mats Hummels kutua Emirates?


Na Oscar Oscar Jr

Pamoja na kuwa kuna taarifa za klabu ya Manchester United kuhusishwa na uhamisho wa beki bora wa kimataifa wa Ujerumani Mats Hummels, kuna habari zimetolewa leo hii kuwa klabu ya Arsenal iko karibu sana kumnasa beki huyo kisiki ambaye alikuwa msaada kwa timu ya taifa ya Ujerumani kutwaa Ubingwa wa dunia nchini Brazil.

Arsenal wanategemea uwepo wa walinzi wao, Per Martesacker na Laurent Konscienly kwa kiasi kikubwa, kufuatia kuuzwa kwa Nahodha wa timu hiyo, Thomas Vamerleen aliyejiunga na timu ya Barcelona ya nchini Hispania. 

Mmoja wa mabeki hao anapokuwa majeruhu, Wenger amelazimika kumtumia Nacho Monreal na Calum Chambers kwa nyakati tofauti.

Katika michezo tisa ya ligi kuu nchini Uingereza, Arsenal wamesharuhusu kufungwa magoli 11 na Hummels, anaonekana kuwa mtu sahihi kuziba mapungufu hayo. 

Mara kadhaa kocha wa Arsenal amekuwa akiwataka wachezaji wengi bora lakini, amekuwa mbahili kutoa pesa nyingi katika manunuzi na hata kulipa mshahara kiduchu.

Hummels anadaiwa kuigharimu Arsenal kiasi cha Pauni 31.5 lakini, kuna uwezekano Arsene Wenger akashindwa kumnunua kwa madai kuwa pesa hizo ni nyingi. 

Hummels ameeleza kuwa, anatamani kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine lakini ni lazima iwe timu yenye kiwango bora kama Borussia Dortimund na Arsenal, inaonekana kama mahali sahihi kwake.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!