Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 October 2014
Friday, October 31, 2014

Steven Gerrard kutimkia klabu nyingine na kuiacha Liverpool


Na Oscar Oscar Jr

Kiungo mstaafu wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Liverpool, Steven Gerrard ameibuka na kusema kuwa, anaweza kuachana na Liverpool mwishoni mwa msimu huu na kutafuta timu nyingine. 

Mkataba wa kiungo huyo 34 na Liverpool, unamalizika mwishoni mwa msimu huu na hakuna mazungumzo yoyote ya mkataba mpya yaliyofanyika.

Gerrard ambaye anakaribia kufikisha michezo 700 akiwa na jezi ya Liverpool, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kustaafu mwishoni mwa msimu huu na endapo Liverpool hawatomuongezea mkataba, atakwenda kujiunga na timu nyingine.

Gerrard alikuwa moja ya wachezaji waliocheza vema sana msimu uliopita huku akifunga magoli 13 na kutengeneza mengine 15 akitokea eneo la kiungo na kuirejesha Liverpool kwenye michuano ya Ulaya baada ya kumaliza ligi kwenye nafasi ya pili.

Steven huenda akafuata nyayo za kiungo mwenzake wa kimataifa wa Uingereza, Frank Lampard ambaye baada ya klabu ya  Chelsea kutohitaji huduma yake, alikwenda zake Marekani ingawa kwa sasa yuko kwenye klabu ya Manchester City.

Wakati Chelsea walipokutana na Manchester City msimu huu, Frank Lampard alifunga bao la kusawazisha na kufanya mchezo umalizike kwa sare ya 1-1. Nawaza siku ambayo Steven Gerard ataifunga Liverpool huku akiwa na jezi ya timu pinzani, sipati jibu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!