Na Chikoti Cico
Mshambuliaji wa Chelsea aliyeko kwa mkopo nchini Italia akiichezea klabu ya AC Milan, Fernando Torres akaribia kutua kwenye timu yake ya zamani ya Atletico Madrid, hii ni baada ya kuwa na wakati mgumu kwenye ligi ya Seria A ambako mpaka sasa amefunga goli moja tu toka asajiliwe kwa mkopo mapema mwezi Agasti.
Taarifa kutoka kwa kocha msaidizi wa timu ya Atletico Madrid German Burgos zilisema Torres maarufu kama “el nino” ambaye safari ya maisha yake ya soka ilianzia Atletico anakaribia kutua kwenye timu hiyo kwa mara ya pili.
Kocha huyo alikaririwa na vyombo vya habari vya Hispania akisema “Linakaribia (Dili la Torres) kwenye hatua za kumalizika na tunasubiria mambo kukaa sawa, atatuongezea nguvu muhimu kwenye nusu ya pili ya msimu, tutamwezesha kuwa bora kama wengine na anajua wapi anapokuja”
Winga wa Atletico Madrid, Alessio Cerci anatarajiwa kwenda AC Milan kwa mkopo kama sehemu ya dili la Torres ambapo dili hilo litakuwa mpaka mwisho wa msimu wa 2015/2016.
0 comments:
Post a Comment