Arsenal inaweza kuchukua ubingwa wa Uingereza msimu huu
Na Rossa Kabwine
Klabu ya Arsenal inaweza kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu, kama watamsajili kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani, Sami Khedira katika dirisha dogo la usajili la Januari. Hii ni kauli ya winga wa zamani wa arsenal, Perry Groves.
Khedira ambaye yupo katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake na timu yake ya sasa ya real Madrid, anadaiwa kuondoka klabuni hapo ingawa kocha wa timu hiyo, Carlo Ancelotti amesisitiza kuwa, kuna makubaliano yanaendelea kuhusu mchezaji huyo na klabu yake.
Khedira mwenye miaka 27 amekuwa akihusishwa kununuliwa na baadhi ya vilabu vya Uingereza ambavyo ni Arsenal, Chelsea, Manchester City na Manchester United kwa nyakati tofauti.
Arsene Wenger amekuwa katika harakati za kumsajili kiungo huyo tangu dirisha kubwa la usajiri lililopita lakini, madai ya mshahara mkubwa kwa mchezaji huyo ndiyo yaliyokuwa kikwazo.
Kwa sasa inadaiwa kuwa, Khedira amepunguza mshahara wake hadi kufikia pauni 80,000 kwa wiki na Groves anaamini kuwa kiungo huyo anaweza kuifanya Arsenal ikawa sawasawa na timu za Manchester city na Chelsea.
Groves aliuambia mtandao wa Standard Sports kuwa “arsenal wanahitaji kuimarisha sehemu ya kiungo mkabaji na mtu aliye katika akili yake ni Khedira”
Grove alieongeza kuwa, Khedira anaijua kazi hiyo vizuri ana nguvu na uwezo mzuri wakupiga pasi zenye uhakika na haitamchukua muda mrefu kuendana na mazingira ya Arsenal kwasababu, atakuwa na Wajerumani wenzie wanaocheza katika klabu hiyo ambao ni Mesut Ozil, Per Matesacker na Lucas Poldoski.
Arsenal iliyo myuma ya Chelsea kwa pointi tisa, katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza huku Arsene Wenger akipingwa kwa kubadilisha nfumo kutoka 4-2-3-1 na kwenda 4-1-4-1 msimu huu, Arsenal wamekosa kiungo mkabaji kwa muda sasa.
Groves aliyeichezea arsenal mechi 203 katika miaka sita akiitumikia klabu hiyo hadi mwaka 1992, anaamini kuwa wachezaji wa arsenal, bado wana hangaika kuendana na mfumo huo mpya.
0 comments:
Post a Comment