Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 November 2014
Friday, November 28, 2014

Falcao na Marcos Rojo wako fiti kuwavaa Hull City.


 Na Oscar Oscar Jr

Mshambuliaji Radamel Falcao na beki Marcos Rojo wa Manchester United, wamejerea kutoka majeruhi na kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo Loius Van Gaal, wachezaji hao wako fiti na wanaweza kucheza kwenye mechi ya ligi kuu siku ya Jumapili dhidi ya timu ya Hull City.

Bado hali ya beki Luke Shaw haijatengemaa na kuna uwezekana mkubwa asijerejee dimbani mpaka mwakani. Mlinzi huyo wa kushoto aliteguka tena wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Arsenal mchezo uliopigwa ndani ya dimba la Emirates.

Falcao ambaye msimu huu ameanza mechi tatu tu huku akifunga bao moja pekee, amekosekana kwenye mechi nne zilizopita za Manchester United na sasa, anatarajiwa kung'aa dimbani ili kuushawishi uongozi wa Manchester kuweza kumpatia mkataba wa kudumu kutoka klabu ya Monaco.

Kumkosa Daley Blind na kumpelekawa kwa mkopo kwa beki Reece James kule Rotherham, kunamuacha kocha Loius Van Gaal kubakia na Tyler Blackett na Ashley Young, kama wachezaji wa kumuokoa katika safu ya Ulinzi.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!