Podolski kutimka kwa mzee Wenger
Na Oscar Oscar Jr
Lukas Podolski ni moja kati ya washambuliaji ambao walipotangazwa kujiunga na Arsenal, mashabiki wa timu hiyo waliamini kuwa tatizo la mfungaji lingemalizika.
Kutokana na mshambuliaji huyo kupata majeruhi mara kwa mara na kupangwa nafasi za pembeni badala ya katikati kama mshambuliaji, kumemfanya ashindwe kung'aa ndani ya Emirates.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani, anakaribia kuondoka kwenye ya Arsenal huku taarifa zikisema mabingwa wa Italia Juventus wanataka huduma zake.
Madai ya kuwa hana nafasi tena ndani ya Arsenal yaliongezeka pale alipochujwa kwenye kikosi kilicho toka sare ya 2-2 dhidi ya Everton Jumamosi.
Badalake, Podolski alisafiri kwenda Ujerumani kutizama klabu yake ya zamani, Cologne ikitoka sare tasa na Hamburg huku taarifa zaidi zikisema hatarejea London kusini tena.
Inaaminika Juventus wamewasilisha ombi la pauni milioni 10 kusajili mshambuliaji huyo, 29, kutoka Arsenal baada ya mpango wa kumpata kwa mkopo nchini Italia kutibuka.
0 comments:
Post a Comment